Lamentations 5


1 aKumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata,
tazama, nawe uione aibu yetu.

2 bUrithi wetu umegeuziwa kwa wageni,
na nyumba zetu kwa wageni.

3 cTumekuwa yatima wasio na baba,
mama zetu wamekuwa kama wajane.

4 dNi lazima tununue maji tunayokunywa,
kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.

5 eWanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu,
tumechoka na hakuna pumziko.

6 fTumejitolea kwa Misri na Ashuru
tupate chakula cha kutosha.

7 gBaba zetu walitenda dhambi na hawapo tena,
na sisi tunachukua adhabu yao.

8 hWatumwa wanatutawala
na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.

9 Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu
kwa sababu ya upanga jangwani.

10 iNgozi yetu ina joto kama tanuru,
kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.

11 jWanawake wametendwa jeuri katika Sayuni,
na mabikira katika miji ya Yuda.

12 Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao,
wazee hawapewi heshima.

13 kVijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia,
wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.

14 lWazee wameondoka langoni la mji,
vijana wameacha kuimba nyimbo zao.

15 mFuraha imeondoka mioyoni mwetu,
kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.

16 nTaji imeanguka kutoka kichwani petu.
Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!

17 oKwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia,
kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,

18 pkwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa,
nao mbweha wanatembea juu yake.

19 qWewe, Ee Bwana unatawala milele,
kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi.

20 rKwa nini watusahau siku zote?
Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu?

21 sTurudishe kwako mwenyewe, Ee Bwana,
ili tupate kurudi.
Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale,

22 tisipokuwa uwe umetukataa kabisa
na umetukasirikia pasipo kipimo.
Copyright information for SwhKC